Description
MATUMIZI
Tumia uwiano wa 1:4, yaani 1 toroli/ ndoo ya saruji kwa 4 toroli/ndoo ya mchanga halafu changanya mpaka rangi ya mchanganyiko iwe na mwonekano unaofanana kwa kazi zote kama ilivyoelezwa awali.
KUMBUKA 01: Tumia kifaa kinachofanana (ndoo au toroli) kupimia mchanga
na saruji.
KUMBUKA 02: Ubora wa mchanganyiko inategemeana na ubora wa mchanga pamoja na maji.
VIFAA KINGA
- Vumbi la saruji kwenye ngozi yenye unyevunyevu au jicho linaweza kuleta madhara.
- Jilinde kwa kuvaa vifaa vya usalama vinavyofaa.
- Ikiwa saruji imegusana na ngozi au jicho, osha mara moja kwa maji.
- Hifadhi saruji mbali na watoto.
UBEBAJI
Nyanyua kwa uangalifu ili kupunguza hatari ya kuumia wakati wa ubebaji.
UHIFADHI
- Hifadhi mfuko wa saruji kwenye jukwaa lililoinuliwa ndani ya chumba kisichokuwa na unyevu, na kama hii haiwezekani hifadhi saruji kwenye jukwaa lililoinuliwa kisha uifunike kwa karatasi ya kuzuia maji.
- Saruji itumike kufuatana na siku iliyohifadhiwa kumaanisha ya kwanza kuhifadhiwa iwe ya kwanza kutumika kwa sababu saruji inatabia ya kuganda ikikaa kwa muda mrefu.



